×

Mchimbaji Mdogo wa Tanzanite Manyara Awa Bilionea – Video

MCHIMBAJI mdogo wa madini ya Tanzanite, Saniniu Laizer, leo Juni 24, 2020, amekuwa bilionea baada ya  kuiuzia serikali  mawe mawili makubwa ya Tanzania yenye thamani ya Tsh. bilioni 7.8 yakiwa na uzito wa kilo 14.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Madini,  Profesa Simon Msanjila,  amesema mawe hayo mawili, moja lina kilo 9.2 na thamani ya sh. bil. 4.5, la pili  kilo 5.8 la bil. 3.3.

 

“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni, kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo,” amesema Prof. Msanjila

Ameongeza kuwa sekta ya madini ina uwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka hivyo panahitajika uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.

Leave a Comment