×

Molinga Aiokoa Yanga SC Taifa – Video

YANGA jana Jumatano ikicheza Uwanja wa Taifa jijini Dar dhidi ya Namungo FC, iliokolewa isipate kipigo na straika wake, David Molina baada ya kufunga mabao mawili na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-2.

 

Katika mchezo huo ulioanza majira ya saa 1:00 usiku, Yanga ilitengeneza mashambulizi mengi kipindi cha kwanza, lakini hayakuwa na madhara.Kipindi cha pili ndiyo kilizaa mabao ambapo Namungo ilianza kufunga kupitia kwa Charles Edward dakika ya 53 na 71, kabla ya Molinga kutokea benchi na kusawazisha dakika ya 80 na 90+6.

Sare hiyo inaifanya Yanga kuendelea kusalia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 57 nyuma ya Azam yenye 58 na Simba 78.


Mashabiki wa Yanga ambao wanaonekana kama kukata tamaa na timu yao, jana walijitokeza wachache uwanjani hapo, huku gumzo kubwa likiwa ni kitendo cha kiungo wao, Bernard Morrison kuzungumza kuhusu mustakabali wake ndani ya klabu hiyo ambao uliwakera sana.

 

Kwa matokeo ya kukosa pointi tatu jana kwa Yanga na Azam, inamaanisha Simba inahitaji ushindi wa mechi moja tu kuwa mabingwa wa msimu huu.

STORI: WILBERT MOLANDI,DAR ES SALAAM

Leave a Comment