×

Mkuu Kitengo Tehama Global Group Auacha Ukapera

Mkuu wa Kitengo cha Tehama cha Global Publishers, Edwin Lindege  akiwa katika pozi na mkewe, Litha Mwinuka, katika ufukwe wa Ziwa Victoria huko Kahunda, Sengerema.
Bi harusi, Litha Mwinuka,  akimvisha pete mmewe, Edwin Lindege, katika kanisa Katoliki Parokia ya Mwangika, Sengerema, Mwanza.
Bi harusi na bwana harusi wakila kiapo kutoka kwa padri wa Parokia ya Mwangika.
 Lindege akisaini cheti cha  ndoa.
Bi harusi akisaini cheti cha ndoa kama ishara ya kufunga pingu za maisha.
Edwin  na Litha  wakionyesha vyeti vyao baada ya kufunga pingu za maisha.
Picha ya pamoja ya wazazi wa bwana  na bi harusi.
Wanandoa wakitoka kanisani mara baada ya kufunga ndoa.
Picha ya ndugu wa bwana na bi harusi katika ufukwe wa Ziwa Victoria.

 

MKUU wa kitengo cha Tehama cha Kampuni ya Global Publishers, Edwin Lindege, ameuacha ukapera baada ya kufunga pingu za maisha na mkewe, Litha Mwinuka, katika kanisa la Mwangika, Sengerema mkoani Mwanza.

 

Ndoa hiyo ilifuatiwa na shamrashamra mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupiga picha za kumbukumbu katika ufukwe wa Ziwa Victoria huko Kahunda, Sengerema, Mwanza.

 

 

Leave a Comment