×

Timu Championi Watoa Neno Kwa Atakayeshinda Gari

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group, Eric Shigongo.

ZIMESALIA siku tatu tu kwa mshindi wa gari aina ya Toyota FunCargo yenye thamani ya Sh milioni 10 kupatikana.

Gari hilo litapatikana kwa kuponi moja tu kutoka Gazeti la Championi ambalo linauzwa Sh 800 tu au kwenye Gazeti la Spoti Xtra linalouzwa Sh 500 tu.

 

Hivyo, kuelekea droo ya mwisho ya bahati nasibu hiyo iliyopewa jina la Baba Lao itakayofanyika Jumatano ijayo Julai 1, 2020, haya hapa ni maoni ya baadhi ya memba wa timu ya Gazeti la Championi kuelekea droo hiyo ya mwisho:

Eric Shigongo

Mkurugenzi

Bahati nasibu hii ina maana kubwa kwetu Global Publishers, tumekuwa tukirudisha kwa jamii kile tunachokipata, naamini wasomaji ni mashahidi, tumeshawahi kutoa vitu vingi vikubwa ikiwemo nyumba. Tunafanya yote hayo ili kuonyesha tunavyowathamini wasomaji wetu wote bila kuwabagua.

Mkurugenzi wa Global Group Lydia Bukumbi.

Lydia Bukumbi

Mkurugenzi

Magazeti ya michezo bora kwa sasa nchini ni Championi na Spoti Xtra, ubora wake ndiyo ambavyo yanataka kufanya maisha ya wasomaji yawe bora pia, wasomaji wazingatie mashari tu ili mmoja wao ashinde hiyo Toyota Funcargo.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally.

Saleh Ally

Mhariri Mtendaji

Kutoa zawadi yenye thamani ya Sh milioni 10 ni kitu kikubwa sama ambacho Global tunakanya, japo huko nyume tumewahi kufanya mengi makubwa zaidi ya hili lakini maana yetu ni kuonyesha wasomaji kuwa bila wao sisi hatuwezi kufika popote. Wao ndiyo wanatufanya kuwa na gazeti bora kuliko yote Afrika Mashariki na Kati katika michezo na burudani kwa lugha ya Kiswahili.

 

Phillip Nkini

Mhariri Championi Jumatano

Hii ni moja ya njia ya kurudisha kile kidogo tunachokipata kwa wasomaji wetu, Championi tunaamini kuwa wasomaji wetu ni muhimu sana kwa kipindi hiki.

 

Akishinda mmoja, basi ni alama kuwa wasomaji wetu wote kuwa wamekuwa washindi, baada ya hii itakuja zawadi nyingine kubwa zaidi.

 

Lucy Mgina

Mhariri Championi Jumamosi

Unaweza kuona ni kidogo lakini ni kitu kikubwa sana kwani gari hii inaweza kukusaidia kuingiza kipato kwa kuifanya UBER au ikasaidia kazi zingine mbalimbali. Global imefanya hivi ili kurudisha kwa jamii kile kidogo inachopata hasa kipindi hiki cha mtikisiko wa kiuchumi.

Wilbert Molandi

Mwandishi

Wapo watu wengi wenye ndoto za kupata mafanikio kwa muda mrefu, lakini safari hii ya Baba Lao ndoto ya mmoja wao itatimia, ushauri wangu wanunue magazeti ya Championi kwa wingi, kwani mbali na zawadi ya gari zipo nyingine nyingi tu ambazo zitatolewa.

 

Said Ally

Mwandishi

Uzuri ni kwamba kila kitu kipo wazi kama ambavyo wasomaji walivyoona kwenye droo kadhaa nyuma zilizopita, kitu cha muhimu na msingi zaidi wasomaji kujiweka karibu kwa ajili ya kujitengenezea nafasi ya kushinda mkoko huo mpya.

 

Joel Thomas

Mwandishi

Kwa maisha ya Mtanzania wa kawaida kuamka asubuhi na kujikuta ukimiliki gari la milioni 10, si kitu kidogo ni bahati kubwa sana ambayo pasi na shaka inaweza kubadilisha kabisa historia iliyopita ya maisha ya mtu. Naupongeza uongozi wangu kwa hiki unachokifanya, yaani kurudisha kile wanachokipata kwa wasomaji wetu.

 

Marco Mzumbe

Mwandishi

Hatua ya mafanikio ni pamoja na kumiliki kitu chenye thamani kinachoweza kurahisisha baadhi ya mambo na yakanyooka, ukijishindia gari utakuwa umefikia hatua hiyo ya mafanikio kwa kuwa kuna vingi vitabadili maisha yako.

 

Shafii Hashim

Msanifu kurasa

Magazeti ya michezo bora kwa sasa nchini Championi na Spoti Xtra, ndivyo yalivyo bora yanataka kubadili pia maisha yako yaweze kuwa kuwa bora kupitia shindano hili.

 

Khadija Mngwai

Mwandishi

Hii ni bahati nasibu ya kweli kabisa na atakayeshinda  anakabidhiwa ndinga lake bila wasi, hivyo ni juhudi yako kuendelea kununua magazeti ya Championi na Spoti Xtra ili uweze kujiwekea nafasi ya kushinda.

 

Nicolaus Mtakingilwa

Mtaalamu wa IT

Baba Lao ni miongoni mwa zawadi kubwa, hii inafanywa kurudisha kile kidogo kwa wasomaji wake, hivyo siyo ya kuikosa kabisa.

 

Omary Hussein

Mhudumu mgahawani

Championi na Xtra ni magazeti bora ya michezo hapa nchini, hata mtaani tunaliona hilo, hata wateja wetu wengi wa nje wamekuwa wakituthibitishia hilo. Naamini shindano hili litaingeza wateja wengine wengi.

 

Habiba Mtalikwa

Mapokezi

Yaani kama siyo sisi wafanyakazi kuzuiliwa kushiriki, binafsi ningeshiriki (anacheka), roho inaniuma sana kutoshiriki kwenye bahati nasibu hiyo, namtakia kila la kheri atakayeshinda.

Hamisi Mbaske

Mlinzi

Mimi na wenzangu tumekuwa tukipata wageni wengi wanaoleta kuponi wenyewe, wapo wanaofika hapa na kusali, nafikiri hiyo inaonyesha jinsi gani wanavyolitamani hilo gari. Sina ya kusema mengi, nawatakia kila kheri wote.

Anna Mabula

Uhasibu

Tunashukuru Mungu jamii inatuelewa na mrejesho wa hiki kinachofanyika tunauona kupitia mauzo ya magazeti yetu. Tunawashukuru wasomaji wote japo mshindi wa gari atakuwa mmoja, watambue kuwa hiyo ni bahati ya mtu na inaweza kumuangukia yeyote ambaye ametimiza vigezo.

Leave a Comment