
MMEKWISHA! Hivyo ndivyo utakavyoweza kusema, ni baada ya uongozi wa Yanga kuwalipa wachezaji wake mishahara ya miezi miwili sambamba na bonasi zao za mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.
Hiyo yote ni katika kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la FA utakaowakutanisha na watani wa jadi, Simba Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo unaotarajiwa kujaa up-inzani mkubwa, Yanga wataingia uwanjani waki-hitaji rekodi na ushindi ili wavuke hatua ya fainali na kulichukua kombe hilo ili wafuzu kucheza mashindano ya kimataifa, wakati Simba wenyewe wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa ligi.

Championi Jumatatu, lina taarifa kuwa wachezaji hao walilipwa mishahara na bonasi hizo saa chache mara baada ya kuanza safari ya kuelekea Musoma kwenda kucheza na Biashara United.Chanzo hicho kilisema kuwa, lengo la kulipa madai hayo ya wachezaji ni kuwaongezea morali ya kucheza kwa bidii ili wafanikishe ushindi katika mchezo huo wa FA.
“Hakuna mchezaji yeyote anayedai mshahara na bonasi za mechi za ligi na FA, viongozi wameona umuhimu wa mchezo wa nusu fainali watakaokutana na Simba na ndiyo sababu ya kuwalipa mishahara, bonasi wachezaji wetu.
“Sasa hivi wachezaji ndiyo tunawadai wao, kwa kuhakikisha wanafaniki-sha ushindi katika mich-ezo tuliyoibakiza ukiwemo huu wa ligi dhidi ya Bi-ashara kabla ya kumalizia na Kagera Sugar.
yanga
“Uon-gozi unau-chukulia umuhimu mkubwa mch-ezo huo wa FA tutaka-pocheza dhidi ya Simba, hivyo tumekamilisha malipo yao ya mishahara na bonasi, pia uon-gozi hivi sasa unaandaa kambi nzuri ya timu katika kuelekea mchezo wa wa-tani wetu,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuzungumzia hilo, alisema: “Sisi tumeandaa utaratibu mzuri wa malipo ya mishahara ya wachezaji, hivyo katika timu yetu hakuna mchezaji anayedai mshahara wala posho.
WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam