×

Rais Magufuli Ateua DC na Ma-DED Watano

Rais Dkt. John Magufuli leo Julai 07,2020 amemteua Lauteri Kanoni kuwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe akichukua nafasi ya Ally Kasinge, kabla ya uteuzi huo Kanoni alikuwa Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Serikali za Mitaa Mkoa wa Songwe.

 

Aidha, Rais Magufuli amemteua Bashir Mhoja kuwa Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Wilaya ya Iringa akichukua nafasi ya Robert Masunya, Ramadhani Possi kuwa DED wa Chalinze akichukua nafasi ya Amina Kiwanuka, Baraka Michael kuwa DED wa Urambo akichukua nafasi ya Nakainga (amestaafu), John Nchimbi kuwa DED wa Babati na Emmanuel Matinyi kuwa DED wa Kishapu.

 

Leave a Comment