×

Wachezaji wa Stars wakunwa na udhamini wa Serengeti Premium Lager

Wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, wameelezea kufurahishwa na udhamini wa Bia ya Serengeti Premium Lager na kusema kuwa udhamini huo umekuwa chachu kubwa kwa mafanikio ya timu.

Wakizungumzia kuhusu udhamini huo wachezaji hao akiwemo John Bocco, ambaye ni mshambuliaji wa Timu hiyo alisema kuwa udhamini wa Bia ya Serengeti umeiwezesha timu kupiga hatua kubwa ikiwa ni pamoja na kufuzu kucheza Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka jana, baada ya miaka 39 tangu ifuzu mara ya mwisho.

“Mpira unahitaji uwekezaji ili kupata mafanikio. Kampuni ya bia ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti imeweza kutoa udhamini ambao umekuwa chachu kubwa katika kuiimarisha timu yetu ya taifa. Pengine kama siyo udhamini huu tusingeweza kufika hapa tulipofika leo,” alisema.

Kampuni ya SBL kupitia Bia ya Serengeti ilikuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa kuanzia mwaka 2017 baada kusaini mkataba wa miaka 3 na Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa nchini (TFF)

Frank Domayo, kiungo wa timu ya taifa amesema mdhamini pia amefanikiwa kujenga umoja na uzalendo kwa mashabiki jambo ambali limekuwa likiwapa hamasa kubwa wachezaji.

“Mdhamin amefanya kazi kubwa kuwaleta Watanzania pamoja na kuhamasisha uzalendo kwa timu yao ya taifa kupitia vyombo vya habari na kampeni zinazowahusisha wachwzaji moja kwa moja,” alisema.

Kwa upande mwingine Domayo amesema mdhamini amekuwa akifanikisha maandalizi mazuri kwa kuhakikisha kuwa mahitaji ya wachezaji na timu kwa ujumla yanapatikana kwa uhakika na kwa wakati pia.

‘Tumeona tofauti kubwa wakati bia ya Serengeti ikiwa mdhamini wa timu yetu ya taifa. Tumekuwa tukikaa kwenye hoteli nzuri tunaposafiri na tunapokuwa kambini na hata maslahi yetu sisi wachezaji yameboreshwa kwa kiasi kikubwa jambo ambalo limetufanya tujitume zaidi,” amesema

Beki wa kulia wa timu hiyo Erasto Nyoni anasema mdhamini kwa kiasi kikubwa amekuwa karibu na wachezaji jambo ambalo limekuwa likiwatia moyo.

Mdhamini amekuwa na timu siyo tu ndani ya uwanja bali hata nje ya uwanja kwa kutupa hamasa na hili limekuwa likiwajenga vyema wachezaji kisaikolojia,”.

Nae mlinda mlango wa timu hiyo Mechata Mnata alisema mdhamini amekuwa akijitahidi kuipa timu kila aina ya ushirikiano na hivyo kufanya maandalizi yawe mazuri na kuweza kufanya vizuri katika mechi zake

Leave a Comment