
NILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA…
Je, unayafahamu maajabu ya Mto Nile na sababu za maji ya mto huu kutumiwa na Taifa la Misri pekee? Pia unaifahamu mito mirefu zaidi duniani?
Usipate taabu, mambo haya yote utayapata hapa, endelea kunifuatilia.
KAMA nilivyoeleza wiki iliyopita, Mto Nile ni wa pili kwa urefu duniani ukiachana na Mto Amazon kwa mujibu wa Serikali ya Brazil ambayo ndiyo hutoa takwimu hizo.
Mto Nile umepita katika nchi tano Afrika kabla ya kutiririsha maji yake kwenye Bahari ya Mediterenian. Nchi hizo ni; Uganda, Ethiopia, Sudan, Burundi na Misri.
Mto Nile una urefu wa kilomita elfu sita na mia sita sabini (6670km) ambazo ni sawa na maili elfu nne na mia moja sitini (4160miles). Kumbuka 1km=0.6miles
Mto Nile unatiririsha maji yake kwenye Bahari ya Mediterenian iliyopo Kaskazini Mashariki mwa Afrika ambapo unatiririsha wastani wa lita milioni tatu na laki moja (3.1m) za maji kwa sekunde ambazo ni sawa na galoni za maji (680,000).
Asilimia 22% pekee za Mto Nile, ndizo zinahusishwa na nchi ya Misri.
Asili ya Mto Nile ni nchini Tanzania.
Chanzo cha Mto Nile ni mikondo ya maji iliyopo Kaskazini mwa Ziwa Victoria ambalo ndilo ziwa kubwa barani Afrika.
Licha ya kuwa chanzo cha Mto Nile ni Ziwa Victoria, lakini sasa inaaminika kwamba Burundi ndiyo chanzo cha Mto Nile.
Mto Nile umegawanyika katika aina mbili ambazo ni Nile Nyeupe na Nile ya Bluu.
Mito hii miwili inakutana nchini Sudan, lakini chanzo chake ni Ziwa Tana huko nchini Ethiopia.
Nile ya Bluu inachangia asilimia 85% ya Mto Nile wakati Nile Nyeupe ikichangia asilimia 15% pekee. Lakini yote hupeleka maji Mediterenian.
Watu wa kale wa Misri walikua wakiishi kando ya Mto Nile kwa sababu mto huo ulitiririsha maji ya kutosha. Pia bonde la Mto Nile lilikua na rutuba ya kustawisha aina nyingi ya mazao yaliyotumika kwa ajili ya chakula. Mto Nile pia ulitumika kwa ajili ya usafiri.
Kabla ya kujengwa kwa Bwawa la Aswan, mwaka 1960, Mto Nile ulifurika kila mwaka, majira ya Juni hadi Septemba.
Mvua na barafu ndivyo vilifanya Mto Nile kufurika. Bonde la Mto Nile ni kubwa na linahusisha baadhi ya maeneo nchini Tanzania, Burundi, Rwanda, Kongo (DR) na Kenya.
Jina la Nile limetokana na neno la Kigiriki ‘neilos’ lenye maana ya bonde.
Kama hupendi nyoka, basi usikanyage kabisa kwenye Bonde la Mto Nile kwani una aina zaidi ya kumi ya nyoka wenye sumu kali na hata wasio na sumu.
Mto Nile una mamba wenye hasira kali duniani aina ya apex predators, ukiachana na ukali, mamba hawa wana sumu kali yenye kuozesha kwa haraka.
Mto Nile pia una viboko wa kila aina. Bonde la Mto Nile ni maarufu kwa kilimo cha matikiti na mimea aina mbalimbali.
Samaki aina ya tiger wanapatikana kwenye Bonde la Mto Nile pekee barani Afrika. Samaki hawa ni wakorofi na wana meno makali sana.
Kambale wenye futi nne zaidi wanapatikana kwenye bonde hili.
Kwenye kingo za Mto Nile kuna kenge wenye futi tatu za urefu. Kenge hawa ni maarufu kwa kuiba mayai ya mamba na kula nyoka. Samaki aina ya tuna wanapatikana kwenye Bonde la Mto Nile. Samaki hawa wanavunja rekodi ya uzito duniani, kwa kufikisha hadi kilo mia mbili na hamsini 250kg.
Pia Mto Nile una vyura wakubwa wenye sumu kali.
Ukiachana na hayo yote, Mto Nile una ndege na mimea ambayo huwezi kuipata popote duniani.
Mwisho mto nile ni roho ya misri.
Itaendelea wiki ijayo.
MSIMULIAJI; SIFAEL PAUL