
MKUTANO wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wamempitisha Dkt. Hussein Ali Mwinyi Kuwa Mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama hicho. Mkutano huo umefanyika leo Julai 10, 2020 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Dkt. John Magufuli.
“Jumla ya wanachama 32 wamejitokeza kuwania urais (Jamhruri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar) wakiwemo wanawake 5 na wanaume 27, lakini mwanachama mmoja aitwaye Hussein Ibrahim Makungu aliamua kujitoa katika mchakato huo na kubaki wanachama 31.

Akitangaza matokeo ya kura zilizopigwa na wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Spika Job Ndugai, amesema waliopigiwa kura ni Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 16, Dkt Khalid Salum aliyepata 19 na Dkt. Hussein Mwinyi aliyepata kura 129 sawa na asimilia 78.65 na hivyo kumfanya Dkt. Hussein Mwinyi kuchangulia kuwa mgombea urais wa Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kutagazwa kuwa mshindi Dkt. Mwinyi amesema kuwa amepewa heshima kubwa kwa kupata kura 129 na hiyo inaonyesha imani ya watu waliyonayo kwakwe na kuahidi kuwa atafanya kazi kwa kulitumikia Taifa kwa uwezo wake wote.

“Kinachonipa faraja ni kwamba tulikuwa 32 na hatimaye sasa niko mimi wezangu weote wako tayari kushirikiana nami kwa sasa hakuna timu Miwnyi wala timu nyingine bali kuna timu ya chama cha mapinduzi” amesema Mwinyi.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua rasmi na kuipitisha Ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 – 2025 leo Ijumaa, Julai 10, 2020, wakati wa Mkutano wa Halshauri Kuu ya CCM Taifa jijini Dodoma.