×

Zungu Awachana Viongozi Vijana – Video

MBUNGE wa Ilala kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu, amewaasa viongozi vijana kuacha majivuno wanapopewa nafasi hizo na badala yake wawatumikie wananchi kwa unyenyekevu na kufuata misingi ya utawala na sheria za nchi.

 

“Ujana una mambo mengi, kuna kujivuna na ulimbukeni, wakipata vyeo mabega wanapandisha juu, anadharau mpaka vijana wenzake, anataka kuchukua mpaka wake wa wenzake… tumeoma vijana wengi wanatumbuliwa, kimbilieni busara na hekima…”amesema.

 

Amesema hayo leo Jumatatu, Julai 13, 2020 wakati akizungumza kwenye mahojiano katika mahojiano maalum na kipindi cha 255 Front Page kinachoruka kupitia +255 Global Radio na Global TV online.

 

“Kampeni ya kuondoa mifuko ya plastiki imefanikiwa kwa zaidi ya asilimia  tisa  mpaka asilimia mia moja, mwitikio wa wananchi ni mzuri sana, lakini mifuko hii imeanza kurudi tena kutokea nchi jirani, nitoe angalizo, sheria ni kali na watu wataumizwa.

 

“Suala la michanga kujaa kwenye barabara hili ni la halmashauri husika, sisi kama wizara kazi yetu ni ku-monitor  (kufuatilia) wanapokosea tunawakumbusha.

 

“Sera yetu ya mazingira imepitwa na wakati, ni ya miaka kumi na nane iliyopita, lakini tunaandaa sera mpya na hivi karibuni itapelekwa kwenye Baraza la Mawaziri, itahusisha mambo ya tabia za nchi, taka, na waste electronics.

 

“Kwanza hakuna utekelezaji wa mbunge, kuna utekelezaji wa Ilani ya Chama, sisi Ilala tumeweka mikakati ya kuinua vipaji vya soka kwa vijana tumejenga Uwanja wa Benjamin Mkapa zamani ulikuwa mchanga tu sasa unaitwa, Wembley ya Ilala,” amesema Zungu.

 

Leave a Comment