
BILIONEA Mchimbaji wa Madini, Saniniu Laizer, amewasihi Watanzania kuacha kukimbilia mjini badala yake watoke mjini wakafanye shughuli za uchimbaji wa madini na wataona faida yake.
Laizer amesema hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na taasisi zake katika maonyesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam na kumshukuru Rais Magufuli kwa kujenga ukuta wa Mirerani kwani umekuwa na ulinzi mkubwa kwao.