×

Eymael: Adui Yetu Kwa Sasa ni Huyu

BAADA ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amefunguka kwa sasa kitu pekee kilichopo mbele ni kupeleka presha kwa wapinzani wao Azam FC katika kumaliza nafasi ya pili.

 

Mbelgiji huyo amesema kwa sasa hakuna chochote kilichopo mbele yao zaidi ya kupambana kuhakikisha wanamaliza kwenye nafasi hiyo ya pili baada ya malengo yao kushindwa kufikiwa.

 

Kocha huyo alitoa kauli hiyo baada ya Yanga kupoteza mechi yake ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho mbele ya Simba kwa mabao 4-1.

Eymael ameliambia Championi Jumatano, kuwa kwa sasa wataweka presha kwa Azam kwa kushinda mechi zao ikiwemo ya leo Jumatano mbele ya Singida United kwa ajili ya kusogea kwenye nafasi ya pili katika msimamo.“Hakuna ambacho kipo mbele kwa sasa zaidi ya ligi pekee.

 

Tumepoteza mechi yetu na Simba ambayo kwetu ilikuwa muhimu sana ila tukipoteza tunapoteza kama timu na tukishinda ni hivyohivyo.

 

“Kwa sasa tunachotakiwa kufanya ni kuweka presha kubwa kwa Azam kuhakikisha kwamba tunamaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi,” alimaliza Eymael.

Leave a Comment