×

Young Killer Ammwagia Sifa Wolper

Rapa kunako kiwanda cha Hip Hop, Young Killer ammwagia sifa za kumkubali sana aliyekuwa mpenzi wake, mwanama kunako Bongo Muvi Jackiline Wolper.

Young Killer amesema kuwa Wolper ni mwanamke wa kitofauti sana kwani akipenda anapenda kweli kweli, na mbali na hilo pia ni mtafutaji.

“Wolper ni mwanamke mrembo, mbali na urembo pia anajua kupenda maana akikupenda anakupenda kwelikweli, ni mtafutaji anapambana sana, bado naenelea kumkubali maana hatujaachana kwa ugomvi kivile adi tushindwe kuongea au kuendelea kuwasiliana,’’ alisema Young Killer ambaye kwa sasa anatamba na ngoma ya Exclusive Interview.

Leave a Comment