
WAANDAMANAJI hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walisika wakipiga nara dhidi ya Benjamin Netanyahu na kumtaka ajiuzulu wadhifa wake huo na kujitenga kabisa na siasa kutokana kukabiliwa na tuhuma lukuki za ufisadi.
Waandamanaji hao wamesema, Netanyahuu anapaswa kujiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu na kuachana kabisa na siasa kwani anakabiliwa na tuhuma nyingi za ufisadi na kwamba, serikali yake imeshindwa kukabiliana na janga la virusi vya Corona.
Baadhi ya jumbe zilizokuwa zimeandikwa katika mabango ya waandamaji hao ni “Waziri wa Jinai”, Jiuzulu”, na Subira Yetu Imefikia Tamati.
Baadaye maandamanao hayo yaligeuka kuwa ghasia na mapigano baina ya waandamanaji na vikosi vya usalama vya Israe.
Netanyahu na baraza lake la mawaziri wanalaumiwa kwani badala ya kutanguliza mbele matatizo ya kiafya na kiuchumi yanayoisumbua Israel kwa sasa, wameng’ang’ania kusukuma mbele gurudumu la mipango ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina ukiwemo mpango wa kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina.
Baadhi ya duru za Israel zimeripoti kuwa, chama cha Blu na Nyeupe cha Benny Gantz ambacho kinahesabiwa kuwa muitifaki wa Netanyahu katika kuunda serikali na ambaye ni Waziri wa Vita kimeatangaza kuunga mkono maandamano hayo yaliyo dhidi ya Netanyahu, msimamo ambao unaonesha ni kwa jinsi gani serikali ya Waziri Mkuu wa Israel inakabiliwa na mgawanyiko.