×

Hussein Mwinyi: Hatutaki Ushindi wa Malalamiko Zanzibar -Video

MTEULE wa urais visiwani Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema mwaka huu chama hicho kinataka ushindi usio na malalamiko.

 

Amewataka Wazanzibari kujitokeza kwa wingi wakati wa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

 

“Mwaka huu tunataka tupate ushindi usiokuwa na malalamiko yoyote. Ushindi wa kishindo, usiwe ushindi mwembamba ukaleta malalamiko,” amesema Dk. Mwinyi.

 

Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Julai 2020, baada ya kupokewa na kutambulishwa kisiwani Pemba.

Amesema, watu wengi wanamueleza kama si mtu mkali na kwamba hawamuelewi.

 

“Kuna watu wanasema mimi ni mpole, wengine wanasema mimi hawanielewe, nasema mtanielewa. Sijawahi kusikika kwenye vyombo vya habari, mambo yetu yanafanywa siri ndio maana sijawahi kumkaripia mtu hadharani, kazi zetu ni za siri,” amesema Dk. Mwinyi.

 

Amesema, watu watakaokuwa wabadhirifu, wala rushwa na wazembe haweze kwenda nao kwenye serikali yake kwa kuwa, watakuwa kikwazo katika maendeleo.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8

⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment