
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli leo Jumatatu, Julai 20, 2020 amewaapisha viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni wakiwemo wakuu wa Mikoa wakuu wa Wilaya, wakurugenzi pamoja na Makatibu Tawala.
Miongoni mwa mambo aliyoyazungumzia Rais Magufuli ni haya;
“Nilikuwa napata taarifa leo kwamba wagombea wa ubunge na uwakilishi waliochukua fomu kupitia CCM ni 10,367, waliojaza na kurudisha ni 10,321 na ambao hawakurudisha ni hawakurudisha 46, katika nchi nzima.Â
“Ninatumaini viongozi watasiamamia kura za maoni kwa haki bila mizengwe, ninatamani kura zikafanyike kama tulivyofanya kwenye Halmashauri Kuu, zihesabiwe hadharani anayepata zero apate hapo hapo anayepata zote hapo hapo, huu uwazi utaendelea kujenga umoja wa CCM.
Kwa walioapishwa;
“Nitashangaa sana miradi ya maji iache kutekelezwa hapa, iache kukalimika, iwe na wizi wakati walioko mbele ni mwanaume na mwanamama na wote ni Wahandisi. Nitasikitika kwanini niliwaonea wale wawili nikakuchagua wewe.
“Dkt. Seif ni Dokta ‘By Profession’. Amesoma akamaliza akapata PhD Uholanzi akaenda kwenye kituo cha Utafiti Ifakara. Miaka ya nyuma aliomba Ubunge Korongwe, hakuwa na hela wala nini alitaka kuwatumikia wanaKorogwe, akapigwa chini.
“Huyu Dkt. Kijazi, sikumteua kwa sababu kaka yake ni Katibu Mkuu Kiongozi, na hili nataka niliweke wazi undugu ni pembeni, amefanya kazi TANAPA vizuri tu na ndiyo maana nikasema imepatikana fursa akawe Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii..
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
⚫️ VISIT AMAZON: https://www.amazon.com/shop/globaltvo…