
GLOBAL GROUP, ni kampuni inayomiliki, pamoja na makampuni mengine, kampuni ya uchapishaji magazeti – Global Publishers Ltd na runinga ya mtandaoni ya Global TV Online na mitandao yake.
FURSA
GLOBAL GROUP inatoa fursa ya ajira kwa vijana wa Kitanzania wenye shauku na mapenzi ya kufanya kazi kwenye tasnia ya habari, upande wa televisheni ya mtandaoni. Aidha, inatoa fursa ya ajira kwa vijana wa Kitanzania pia mwenye shauku na mapenzi ya kufanyakazi ya utafutaji wateja (Sales & Marketing).
MAELEZO
Vijana wanaotatafutwa, ni wale wenye uwezo na sifa za kiongozi anayeweza kuongoza timu na kuleta mafanikio chanya, katika kitengo cha runinga ya mtandaoni (Online TV) na Masoko (Marketing Dept).
SIFA na ELIMU
Anatafutwa kijana wa kiume (upande wa Online TV), mkazi wa jijini Dar es salaam, mwenye elimu ya uandishi wa habari na anayefuatilia na kujua habari za kila siku (News and Current Affairs). Upande wa masoko, anatakiwa kijana wa kiume au wa kike, mkazi wa jijini Dar es salaam, mwenye elimu ya mauzo na masoko (Sales and Marketing) na anayeongea lugha ya Kiingereza kwa ufasaha.
Kama unadhani una sifa zilizoainishwa hapo juu, fika na CV yako katika ofisi za Global Publishers Ltd zilizopo Sinza Mori, Global Group House, Jirani na HakiArdhi na wasilisha maombi yako. Kwa maelezo, piga Simu: 0715 288627
MENEJA MKUU
GLOBAL GROUP
DAR
Mwisho wa kupokea maombi ni JULAI 26, 2020.