
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dkt. Vincent Mashinji, ameshindwa kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kawe, kwa kupata kura mbili kati ya 475.
Mshindi ni Furaha Jacob aliyepata kura 101 akifuatiwa na Angela Kiziga kura 85 na Askofu Josephat Gwajima kura 79.
Matokeo:
1- Furaha Dominic Jacob – 101
2- Angela Charles Kiziga – 85
3- Josephat Gwajima – 79
4- Benjamin Sitta – 61
5. Kippi Warioba – 3
6. Dkt Vicent Mashinji amepata kura – 2.
7. Mwijaku – 1.