×

Hasunga Kidedea CCM Vwawa, Songwe

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameibuka kidedea baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni wakati wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe.

 

Ameibuka mshindi baada ya kuwamwaga wapinzani wake kwa ushindi wa kura 552 sawa na asilimia 76.4.

 

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo, John Palingo,  ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, amesema kuwa idadi ya wajumbe wa mkutano huo ni 801 lakini wajumbe waliopiga kura ni 736 huku kura 13 zikiwa zimeharibika.

 

Palingo amemtaja Erick Minga aliyepata kura 129 kuwa ndiye aliyeshika nafasi ya pili akifuatiwa na wagombea wengine ambao ni Dismas Haonga- 9, Alex Edward – 7, Augustino Simbeye- 7, Denis Simbeye-1, Faraja Mwambalo- 2, George Ambilikile-3, Jerald Silwimba-0, Jumanne Sichinzya-3, Oscar Magwaza-1, Stanislaus Nsojo- 3, Stephen Mwamengo-1, Christopher Mwawalo- 3, na Chrispin Mwashambwa-0

 

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni kwa tiketi ya CCM apinduzi Jimbo la Vwawa, Hasunga amewashukuru wajumbe kwa kumuamini huku akiwapongeza washindani wake na akisisitiza ulazima wa wagombea wote kuungana pamoja ili kuhakikisha kuwa CCM inashinda uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Songwe.

Leave a Comment