
Baada ya ajali ndege iliyotokea juzi Jumapili, Kaimu Rais wa Korea Kusini Choi Sang-mok ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa.
Katika kituo cha michezo cha eneo la Muan, Korea Kusini waombolezaji waliweka maua meupe, ambayo yanaashiria huzuni katika utamaduni wa Kikorea.

Heshima pia zimetolewa kwa waathirika 179 katika eneo la ajali, ambapo familia zinasubiri kutolewa kwa miili ya wapendwa wao.
Huku kipindi cha maombolezo kinaanza, jiji la Seoul limesitisha kibali cha kampuni ya wasafiri wa baharini ambao waliendelea na fataki zilizopangwa jana usiku kuadhimisha mwaka mpya licha ya kuambiwa wasifanye hivyo kwa sababu ya kutoa heshima kwa wahanga wa ajali hiyo.