
STAA wa Bongo Movies, Kajala Masanja amejikuta akiduwaa baada ya marafiki zake wakiongozwa na shosti yake, Lamatha kumfanyia sapraizi kwenye siku yake ya kuzaliwa, leo Jumatano, Julai 22, 2020.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Kajala amesema hakufahamu kama marafiki zake hao wangemfanyia kwani alikuwa akijiandaa na kikao; “Mimi niliambiwa leo kungekuwa na kikao na watu ninaofanya nao kazi, lakini nimeshangaa nimefika hapa nimefanyiwa sapraizi, kwa kweli sikutegemea kabisa. Sikupanga kufanya sherehe yoyote bali Lamatha aliniambia jana tumgekwenda dinner.
“Binafsi sina tatizo na Wema, ninamshukuru kwa kuni-wish. Nimekuwa na urafiki na Lamatha kwa zaidi ya miaka saba kwa sababu yeye ananifahamu vizuri, anajua ni wakati gani nina furaha, niko kwenye mood mbaya ama nzuri, na anafahamu staili yangu yote ya maisha, kiufupi tunaelewana vizuri.
“Kwa sasa nipo kwenye mahusiano, nina mpenzi ambaye nina date naye, ni serious relationship, siwezi kusema kama nimevalishwa pete wala siwezi kumwanika, ila muda ukifika na kukiwa na uhitaji huo, nitafanya hivyo. Mwanangu Paula ananisumbua sana “mama ukifa sasa hivi utaiacha na nani?”, ninampango mwakani nibebe ujauzito nipate mtoto mwingine, ninatamani sasa kupata mtoto tena,” amesema Kajala.