
WAKATI Ligi Kuu Bara ikiwa inaenda kumalizika kwa msimu huu, Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji fasta tu ameamua kufunga mjadala mapema baada ya kukabidhi majina ya mashine zote anazozitaka kwa mabosi wake.
Kocha huyo ameongeza kwamba, tayari ameshawapa mabosi wake ripoti nzima ya wachezaji ambao anawataka kikosini kwake kwa ajili ya msimu ujao.
Licha ya kutoweka wazi juu ya majina hayo, lakini Spoti Xtra linafahamu kuwa miongoni mwao yupo beki wa kushoto Mnyarwanda, Eric Rutanga na winga Mkongo, Tuisila Kisinda.

Mbelgiji huyo ameliambia Spoti Xtra, kuwa ripoti hiyo imejaa majina ya wachezaji ambao watakuja Yanga kwa ajili ya kuijenga timu hiyo kuhakikisha inakuwa na kikosi bora kwa msimu ujao.
“Tayari tumepeleka ripoti kwa viongozi ya wachezaji ambao tunawahitaji kwa ajili ya kuboresha kikosi chetu kuendana na mapungufu yaliyoonekana msimu huu.
“Tunaamini kuwa yatafanyiwa kazi ili kutengeneza timu bora kwa ajili ya msimu ujao ambayo itakuwa na uwezo mkubwa wa kupam-bana na kufanya vizuri katika ligi,” ali-weka nukta Ey-mael.
Ka-tika hatua nyingine, inaelezwa kuwa Kamati ya Usa-jili ya Yanga tayari imekamilisha kwa asilimia 90 usajili wa baadhi ya wachezaji wanaowahitaji kwa msimu ujao, huku majina ya wanaoachwa yakiwa tayari yame-shafikishwa katika kamati husika, hivyo wanasubiri ligi imalizike ili kila kitu kiwekwe had-harani.
Chanzo kutoka ndani ya Klabu ya Yanga, kimelitonya Spoti Xtra kwamba: “Usajili wa Yanga msimu ujao utakuwa wa kiwango cha hali ya juu kwani tayari mikakati yote imeshafanyika tangu wakati ule ligi imesimama kutokana na corona.
“Kinachosubiriwa hivi sasa ni ligi kumalizika na dirisha kufunguliwa ili mambo mengine yaweze kukamilika kwa kuwa tunahitaji wachezaji wenye viwango zaidi kuja kuitumikia timu yetu.”
STORI: SAID ALLY NA KHADIJA MNGWAI, DAR