×

Wanaswa na Takukuru Wakiwapelekea Fedha Wajumbe

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoani Mara inatarajia kuwahoji wagombea ubunge Viti Maalum sita mkoa wa Mara ambao wanadaiwa kuwa ni vinara waliohusika kutoa rushwa katika chaguzi za Viti Maalum mkoani humo.

 

Mkuu wa Takukuru Mara, Alex Kuhanda, amesema kuwa hadi sasa wanawashikilia watu watano ambao walipewa fedha kutoka kwa wagombea wa ubunge Viti Maalum na Ubunge wa Bunda Mjini.

 

Takukuru mkoa wa Mara inawashikilia na kuwahoji wajumbe watano na wagombea wawili wa nafasi ya Ubunge jimbo la Bunda Mjini kwa tuhuma za kutoa na kupokea rushwa, ambapo watuhumiwa hao kila mmoja wapo alikutwa na kiasi cha shiling laki moja.
“Hadi sasa tunawashikilia wafuasi watano ambao walipewa fedha kutoka kwa wagombea wa Ubunge Viti Maalum, lakini pia tumekamata Tsh mil 3.3 ambazo zilikuwa tayari kupelekwa kwa wajumbe kila mmoja akagawiwe Tsh. laki moja.
“Tulianza tukakawamata watuhumiwa wanne waliokutwa na hizo fedha lakini mmoja alitupa chooni Tsh 70,000 na kukimbia, lakini na yeye tayari tumemkamata,” amesema Alex Kuhanda.

Leave a Comment