
Mama wa mwanamuziki maarufu wa Afro Pop ndani na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platiumuz’ Sanura Kassim ‘Mama Dangote’ amevunja ukimya juu ya tetesi za mrembo, Jihan Dimack ambaye alimposti kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram pamoja na Esma ambaye ni dada wa mwanamuziki huyo kwenye usiku wa Zuchu, kitu ambacho wananzengo walikitolea macho.
Gazeti hili lilifanya jitihada ya moja kwa moja za kuwatafuta na kufanya mahojiano na mama huyo ambaye watu wengi walitamani kusikia chochote kutoka kwake kwa sababu hata baada ya kumposti alinyamaza kimya na kuwaacha watu wa kwenye mitandao ndiyo waanze kuchokonoa ya hapa na pale.
MSIKIE MAMA DANGOTE HAPA
Ijumaa: Shikamoo mama!
Mama Dangote: Marahaba vipi hali, niambie una mpya gani maana nikiona simu zenu tu najiaanda.
Ijumaa: Hakuna jipya mama yangu ni yale yale tu.
Mama Dangote: Haya nakusikiliza sasa…
Ijumaa: Kwenye akaunti yako ya Instagram umemposti mrembo Jihan, kitu ambacho kimefanya watu wengi wajiulize maswali tele, kuhusiana na kuposti picha ile kwa sababu hata Esma kamposti…
Mama Dangote: Kwanza nataka watu wajue, hakuna mtu wa kunipangia niposti nini, kwa sababu hakuna anayeninunulia bando, aliyenunulia simu, hivyo namposti mtu yeyote ambaye napenda nimposti.
Ijumaa: Kwa hiyo uliamua kumposti Jihan kwa siku hiyo?

Mama Dangote: Sasa nimemposti kwa vile kapendeza na kavaa kama mimi navyopendaga kuvaa na watu ambao wanashindwa kusifia wenzao ni roho mbaya hasa wanawake, kama Shamte, kamposti Wema, ndio kaona yeye kapendeza sasa kwa nini wanikomalie mimi?
Ijumaa: Kwa sababu wameona pia na Esma kamposti waakanza kupata wasiwasi, labda ndiye mkwe mtarajiwa maana Diamond yupo singo kwa sasa?
Mama Dangote: Jamani hivi wanamuona Diamond ndiye anapenda sana wanawake au vipi au ndiye mwanaume peke yake duniani au inakuaje jamani?
Ijumaa: Lakini wewe na Jihan mnafahamiana?
Mama Dangote: Yaani hata ukimuuliza yeye hatujawahi hata kuzungumza, nilimuona siku moja tu alikuja kwenye birthday yangu na sijawahi kumuona tena na hata huyo Diamond sijui kama wana mazoea kabisa.
Ijumaa: Kwa hiyo unawaambiaje watu wenye kusemasema kwenye mitandao huko?
Mama Dangote: Nawasisitiza wasinipangie nani wa kumposti hata kidogo ninatumia bando langu, alafu yule dada kapendeza na ni mrembo.
Baada ya gazeti kuzungumza na mama Dangote, lilimtafuta Esma ambaye ni dada wa Diamond na alipoulizwa kuhusu hilo alifunguka kama ifuatavyo;
“Unajua Diamond ni mtu mzima na ana maamuzi yake. Pia sasa hivi yupo single kwa hiyo siyo mbaya kama akiamua kuwa na mtu, halafu sisi huwa tunamkubali kila mwanamke anayekuja kumtambulisha kwetu, ila hayo mambo ya kuwa ndiye wifi yetu, sio kweli, nilimposti kama mtu ninayemfahamu basi,” alisema Esma.
Jihan Dimachk ni mrembo aliyewahi kuwa Miss Ilala mwaka 2014 na mwaka huohuo akaibuka mshindi wa tatu Miss Tanzania na 2016 aliibuka kidedea baada ya kunyakua Taji la Urembo la Miss Universe ambalo shindalo hilo lilifanyika nchini hapa.
Stori: Imelda Mtema na Memorise Richard, Dar