
KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Sven Vandenbroeck, amekiri kuwa ubora wa safu ya ushambuliaji ya Namungo inayoongozwa na Reliants Lusajo na Blaise Bigirimana ni miongoni mwa vitu vinavyompa hofu kuelekea mchezo wao wa fainali ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kupigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa, Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
Lusajo na Bigirimana msimu huu wameifungia Namungo mabao 22, hivyo kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa timu zenye safu bora ya ushambuliaji ndani ya Ligi Kuu Bara.
Akiuzungumzia mchezo huo, Sven alisema: “Licha ya kwamba timu yetu inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye fainali ya FA dhidi ya Namungo kutokana na ubora tulionao lakini kwa upande wangu natarajia kuwa mchezo huu utakuwa mgumu hasa kutokana na ukweli kwamba Namungo ni timu iliyojengwa vizuri.
“Wana safu ya kiungo iliyo bora na kuna wale washambuliaji wao wawili, Reliants Lusajo na Bigirimana Blaise ambao ni hatari sana hivyo hatupaswi kuwapa nafasi hata kidogo.”
AFUNGAJI BORA
Kagere – Simba Sc 22
Mhilu – Kagera Sugar 13
Wazir Jr – Mbao Fc 13
Mapunda – Mbeya City 12
Lusajo – Namungo Fc 12
Chirwa – Azam Fc 12
Nonga – Lipuli Fc 11
Saliboko – Lipuli Fc 11
Blaise – Namungo Fc 11
Molinga – Yanga Sc 11.
JOEL THOMAS | Dar es Salaam