×

Mzungu Yanga Akubali Muziki wa Kagere, Kahata

LUC Eymael, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa nyota wa Simba, Meddie Kagere na Francis Kahata ni miongoni mwa nguzo imara ambazo zimefanikisha mafanikio ya kikosi hicho kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Kabla ya mchezo wa jana kati ya Polisi Tanzania na Simba uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika Moshi, wachezaji hao walikuwa wamehusika kwenye jumla ya mabao 40 ya Simba kati ya 76 yaliyofungwa kwenye mechi 37.

 

Kagere, raia wa Rwanda, alikuwa amefunga mabao 22 na pasi sita za mabao huku Kahata raia wa Kenya, akiwa amefunga mabao manne na pasi nane za mabao.

 

Eymael ameliambia Championi Jumatatu kuwa: “Kagere na Kahata ni wachezaji wazuri ndani ya Simba kwani wamekuwa wakitimiza majukumu yao na huwa inakuwa ngumu pia kwa Simba kucheza bila hao, hivyo kwenye mafanikio yao nao huwezi kuwaacha.”

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave a Comment