
MENEJA wa kimataifa wa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na WCB, Sallam Sk, amebainisha kwamba kutokana na uwekezaji mkubwa walioufanya kwa msanii wao mpya, Zuchu, promota akimtaka muimbaji huyo aandae Tsh milioni 20 kwa shoo moja.
Kupitia Insta Live, Sallam amedai muimbaji huyo hana hata mwaka kwenye muziki lakini uwekezaji walioufanya ni mkubwa.
Zuchu ambaye ni mtoto wa mwanamuziki wa taarab, Khadija Omary Kopa, amekuwa miongoni mwa wasanii wachache waliokubalika zaidi kwa mashabiki na kupata mafanikio makubwa ya kimuziki ndani ya muda mfupi.