×

Mtoto Amkosha Rais Magufuli, Amkabidhi Mil 5 – Video

MTOTO mmoja anayesoma katika Shule ya Msingi Somanga mkoani Lindi, Rehema Mikidadi Ngenje,  amemkosha Rais  John  Magufuli wakati akiwa njiani akitokea Mtwara alikokwenda kwa ajili ya mazishi ya rais mstaafu, Benjamin Mkapa.

 

”Shule yetu mbovu sana, madawati hamna, sementi imebomoka, kwanza shule yenyewe mbovu, mabati yote yameshakuwa na kutu, shule yote mbovu, rangi zote zilizopakwa sasa zimefutika, inaitwa Shule ya Msingi Somanga nipo darasa la nne,” alisema mtoto huyo.

 

”Naichangia Shule ya Msingi Somanga TZS Milioni 5. OCD wa hapa hakikisha hizi fedha zinaenda benki na zinapelekwa katika hiyo shule, mkazitumie kweli la sivyo nitakuja nifuatilie,  lakini  shilingi 100,000 ibaki kwa huyu mtoto,” amesema  Magufuli.

 

Leave a Comment