×

Solskjaer Akabidhiwa Bil 417.7 za Usajili

MTENDAJI Mkuu wa Klabu ya Manchester United, Ed Woodward, amekubali kutoa kiasi cha pauni 140m (Sh Bil 417.7) kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer, kuhakikisha anafanya usajili wa kutisha kuelekea msimu ujao.

 

Klabu za Premier tayari zimeanza kufanya usajili baada ya dirisha kufunguliwa Julai 27, mwaka huu huku likitarajiwa kufungwa Oktoba 5, mwaka huu.

Man United itatumia kiasi cha pauni 140m, kwa ajili ya usajili, hii ni baada ya timu hiyo kufanikiwa kuingia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao kutokana na kumaliza nafasi ya tatu ndani ya Premier.Kitendo cha Man United kutinga michuano hiyo ya Ulaya, itakusanya kiasi cha pauni 120m (Sh 358.1).

 

 

Man United katika usajili mipango yao mikubwa ipo kwa Jadon Sancho wa Dortmund ambaye dau lake ni pauni 100m na Jack Grealish kutoka Aston Villa, thamani yake ni pauni 75m.Katika hatua nyingine, Man United wana mpango wa kuwauza nyota wake akiwemo Chris Smalling, Alexis Sanchez, Phil Jones, Jesse Lingard, Diogo Dalot, Timothy Fosu-Mensah na Andreas Pereira.

MANCHESTER, England

Leave a Comment