×

Nandy: Billnass Ndio Kila Kitu Kwangu

SEXY lady kunako Bongo Flevani, Faustina Charles ‘Nandy’ amemshukuru mchumba wake William Lymo ‘Billnass’ kwa sapoti anayompa.

 

Akizumgumza na Risasi Nandy amesema kuwa, Billnass amemsukuma sana na kushirikiana naye kwenye kutimiza ndoto ya kufungua kampuni yake ya Nandy Bridal.

 

“Napenda kumshukuru sana mchumba wangu Billnass kwani ameweza kunisapoti kwenye kutimiza ndoto yangu na tulikuwa hatulali, tunafikiria vitu vingi na mawazo mbalimbali mpaka kufikia lengo ambalo tayari limetimia,’’ alisema Nandy ambaye hivi karibuni amezindua kampuni yake mpya ya Nandy Bridal.

STORI: Happyness Masunga

Leave a Comment