
SIMIYU: Wadau mbalimbali wa kilimo wanaoshiriki na kutembelea Maonyesho ya Kilimo yaNaneNane yanayofanyika kitaifa kwenyeUwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, wameonesha kuvutiwa na huduma mpya ya NBC Shambani ambayoimebuniwa mahususi kuenda sambamba na mahitaji ya huduma za kifedha ya wadauhao.
Akifafanuakuhusu huduma hiyo mpya kwa wadau mbalimbali waliotembelea banda la benki hiyo kwenye maonesho hayo, Mkuu wakitengo cha wateja wadogo na wakati, kutoka benki hiyo Bw Raymond Urassa alisemainalenga wadau wote wanaojihusisha na biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazajiwa pembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo.
“Lengohasa la huduma hii ya NBC Shambani ni kuwasaidia wadau wa kilimo kutimizamalengo yao ya biashara ya kilimo ambapo inatoa fursa kwao kuwa na akauntiya vikundi vya wakulima kama vile AMCOSna vikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja,’’ alisema.
Mbalina kuwawezesha wakulima hao kutunza fedha zao kwa urahisi, Bw UIrassa alizitajabaadhi ya faida za huduma hiyo kwa mkulima mmoja mmoja kuwa ni pamoja namkulima kupata faida kwa salio la akiba linalozidi sh 100,000 na kuendelea hukupia kukiwa hakuna makato ya kila mwezi.

“Akaunti ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezeshakuweka fedha bila ada ya uendeshaji waakaunti huku pia vikundi vikifaidika kwa faida nyingi ikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kilamwezi, kupata taarifa za akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamishafedha wakati wa kulipa wakulima wenyeakaunti NBC,’’ alifafanua.
Wakizungumziahuduma hiyo, baadhi ya wadau wa kilimo walisema imekuja wakati muafaka kwa kuwakwasasa taifa linapitia mageuzi ya kilimo ambayo ustawi wake kwa kiasi kikubwaunategemea uwepo wa huduma bora za kibenki zinaenda sambamba na mahitaji wawadau hao.
“Nimeonakupitia huduma hii mkulima anaweza kuweka na kutoa kiasi chochote cha fedhatena kwa wakati wowote. Huo ni moja ya mfano wa huduma ambazo wadau wa kilimotunahitaji ili kufanikisha miamala yetu wakati wowote hususani tunapofanyamanunuzi ya pembejeo za kilimo au kuhifadhi fedha baada ya kufanya biashara,’’ alisema Bw Emmanuel Rutatora ambae nimkulima kutoka wilaya ya Rorya.
Agosti3, 2020.