×

EXCLUSIVE: Millard Afunguka Bifu za Media vs Wasanii…

 

MTANGAZAJI wa Clouds FM, Millard Ayo, ameeleza namna anavyoumizwa na bifu zinazotokea kati ya wasanii na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini huku akidai kuwa jambo hilo linashusha tasnia ya sanaa na habari na hata wakati mwingine kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wadau wa tasnia hizo.

 

Ayo amesema hayo wakati akipiga stori na Global TV Online wakati wa kumbukumbu ya miaka 20 ya msanii wa Bongo Fleva, mwanadada Lady Jaydee ambaye amekuwa na bifu na Clouds Media Group kwa zaidi ya miaka saba lakini sasa tofauti yao imekwisha na wanafanya kazi pamoja na msanii huyo kiroho safi.

 

“Ujue mimi ni muumini mzuri sana wa amani, sipendi bifu za wasanii na media wala sikuwa nafurahia nyimbo za dada yetu kutopigwa Clouds, lakini haya ni mambo ya wakubwa zetu na mimi ni mtu mdogo sana, kwa hiyo nisingeweza kufanya chochote, kwa sasa nina amani na furaha tele kwa Dada Mkuu Jide kurejea tena kufanya kazi na CMG, ndiyo maana nimefanya naye interview tena kwa furaha sana.

 

“Mimi huwa najiwekea malengo kwa mwaka nataka nifanye nini, nimeorodhesha na nimebandika ukutani nyumbani kwangu, hii inanisaidia kila ninapoona ninakumbuka na kuamsha mori ya kufanya kazi kwa nguvu, na kinachonisukuma zaidi ni passion ya kile nachokifanya, lazima upende unachokifanya hata kama hakikulipi, utakifanya vizuri na mafanikio utayapata mbeleni.

 

“Wakati naanza kazi mwaka 2005 kwenye kituo kimoja cha radio nilikuwa nikilipwa Tsh 5,000 kwa wiki sawa na Tsh 20,000 kwa mwezi, sikuwahi kufikisha Tsh 100,000 kwa mwezi ndani ya miaka mitatu hadi mwaka 2008.  Lakini si kwamba ninalalamika, nilikuwa nafanya kazi kubwa sana lakini wengi wetu tunafanya kazi kubwa tofauti na vipato tunavyopata.  Radio ile ilinifundisha vitu vingi sana; experience waliyonipa leo hii wakiniambia niwalipe siwezi, ni gharama kubwa mno,” amesema.

 

Leave a Comment