KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas ametembelea eneo la Mtumba Dodoma kukagua viwanja alivyoahidi Rais Magufuli kwa wachezaji wa Taifa Stars, bondia Hassan Mwakinyo na baadhi ya viongozi wao na kusema hati za viwanja hivyo ziko tayari.

“Nimetembelea eneo la Mtumba leo kukagua viwanja alivyoahidi Rais Magufuli kwa wachezaji wa Taifa Stars, bondia Hassan Mwakinyo na baadhi ya viongozi wao. Viwanja viko eneo zuri, mita 300 kutoka Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Dodoma.

“Hati ziko tayari tunakwenda kuwakabidhi vijana mali yao na zawadi yao kutoka kwa Rais na kutoka kwa Watanzania, Asanteni,” amesema Dkt. Abbas.