
DAR ES SALAAM: Staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amempa makavu mtu aliyedukua akaunti yake ya Mtandao wa Instagram akimwambia kwamba, hata kama amefanya hivyo bado maisha yataendelea kwani chuki na wivu katika maisha yake huwa havina nafasi.

Shamsa aliliambia Wikienda kuwa yeye anafanya kila awezalo kuhakikisha akaunti hiyo iliyokuwa na followers milioni 2.1, inarudi lakini hata asipofanikiwa bado haitamsumbua kwani atafungua nyingine na ana uhakika mashabiki wake wote waliomfuata watarudi tu.

“Kilichofanyika ni chuki binafsi lakini ninaamini kuwa mimi ni kipenzi cha watu, najua nitafungua nyingine na wala mtu huyo asidhani kwamba amenikomoa,” alisema Shamsa.