
MCHEZAJI wa Klabu ya Aston Villa na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Ali Samatta, ameendelea kujitapa kuwa yeye ndiye mbabe wa mchezo wao wa soka dhidi ya Alikiba huku akiwa na historia ya kushinda michezo mitatu waliyocheza kwa misimu mitatu pia.
Samatta amesema kuwa Alikiba amekuwa mtu wa kulalamika kuhusu marefa akidai kuwa marefa wanahongwa ili afungwe.
“Nimemwambia Alikiba atafute refa wake hata mdogo wake. Abdukiba. akichezesha ntamfunga tu,” amesema Samatta.