×

Simba Yatangaza Usajili Kabambe

IMEBAINIKA kuwa baada ya Simba kumalizana na usajili wa wachezaji wawili David Kameta na Charles Ilanfya, timu hiyo haina mpango wa kuongeza usajili wa wachezaji wengine wanaocheza ligi ya ndani.

 

Inasemekana kuwa uongozi wa Simba umeshakamilisha usajili wa beki wa kulia Kameta kutoka Lipuli na mshambuliaji Ilanfya kutoka KMC, wote kwa mikataba ya miaka miwili.

 

Chanzo cha kuaminika ndani ya Simba kililiambia Championi Jumatano kuwa baada ya kumalizana na wachezaji hao Simba haitakuwa na mpango wa kusajili mchezaji mwingine wa ndani na badala yake watageukia usajili wa wachezaji wa kimataifa.

“Simba kwa sasa tutaangalia zaidi usajili wa wachezaji wetu wa kimataifa, kuhusu wachezaji wazawa sidhani kama Simba itaongeza wachezaji wengine, maana hata tulionao unaona jinsi gani wapo kwenye kiwango bora.

 

“Kitu ambacho kilikuwa kinatufanya tusiweze kufanya mambo mengine ni fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, lakini baada ya kumalizika mambo yatakuwa sawa na tutakuwa kwenye mambo ya usajili,” kilisema chanzo.

 

Naye Ofi sa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa: “Simba msimu huu itasajili wachezaji wasiopungua watano ambapo kama tutasajili wawili wa kimataifa basi wazawa watakuwa watatu na kama watatu wakiwa wakimataifa basi wawaili watakuwa wazawa,” alisema Manara.

STORI: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

Leave a Comment