×

Kisa Barakoa; Wananchi Waadhibiwa Usiku Uwanjani


BAADHI ya wananchi wa Rwanda wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kupewa adhabu ya kukaa saa kadhaa na kusikiliza hotuba, na matangazo mbalimbali kuhusu ugonjwa wa  Covid-19 katika uwanja wa michezo wa Nyamirambo, mjini Kigali nchini humo — wakati wa usiku.

Adhabu hiyo imetolewa kwa wananchi hao baada ya kukiuka sheria ya kupambana na Covid-19, walipokutwa wakitembea mitaani bila kuvaa barakoa, kama ambavyo sheria ya nchi hiyo inavyotaka ikiwa ni moja ya njia za kupambana na ugonjwa huo wa mlipuko.

Leave a Comment