Watu 8 wamefariki dunia baada ya kusambuliwa kwa risasi katika hifadhi ya twiga katika Mkoa wa Koure. Waliopoteza maisha ni Wafaransa 6, dereva pamoja na muongozaji wa safari.

Kwa mujibu wa Gavana wa Tillaberi, Tidjani Ibrahim watuhumiwa waliokuwa kwenye pikipiki waliwashambulia kwa risasi walipokuwa katika eneo hilo ambalo ni kivutio kikubwa cha watalii.

Bado hakuna kundi ambalo limekiri kuhusika na shambulio hilo hadi sasa lakini kumekuwa na ongezeko wa mashambulio yanayofanywa na makundi ya Jihad nchini Niger.
