
Watu 5 wamefikishwa Mahakamani kwa makosa 16 likiwemo la kujipatia fedha zaidi ya Tsh. Milioni 10 kwa njia isiyo halali na kufanya utapeli kwa kutumia majina ya taasisi za Salma Kikwete na Mo Dewji Foundation kwenye Mtandao wa Facebook.
Watuhumiwa hao ni Raphael John Kipingiri, Werasoni Tabu Ngedenge, Luck Paschal Paul, Musa Michael Masami na Richard Masalu Richard.
Wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ya mwaka 2020 kwani kwa nyakati tofauti walitenda makosa ya kula njama na kufanya uharifu, kurasimisha uongo, kujipatia fedha isivyo halali, kutumia taarifa za wateja za usajili wa laini pamoja na utakatishaji fedha.
Watanzania wameshauriwa kutopenda kujipatia fedha kwa njia ya mkato kwani matapeli wengi hufanikisha adhima yao kutokana na watu wengi kujipatia pesa kiurahisi hali inayowafanya watapeliwe kirahisi.