×

JPM Awaasa Viongozi wa Dini Uchaguzi Mkuu 2020

RAIS John P Magufuli, ametoa wito kwa viongozi wote wa dini nchini kutumia nafasi waliyonayo kuwahimiza waumini wao kushiriki katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba hasa kwenye kupiga kura.

 

Ametoa wito huu leo Agosti 14, 2020, wakati akizungumza na viongozi wa dini katika Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Kanisa la Tanzania Assemblies God (TAG), jijini Dodoma, ambapo amesema uchaguzi wa mwaka huu utafanyika katika siku ya kazi na siku hiyo itakuwa siku ya mapumziko.

 

“Napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa viongozi wote wa dini nchini kutoa nafasi mliyonayo kuwahimiza waumini wenu kushiriki kwenye uchaguzi huu, hasa kushiriki siku ya kupiga kura na bahati nzuri haitakuwa Jumamosi ,wala Ijumaa wala Jumapili, itakuwa siku ya kazi na siku hiyo itakuwa siku ya mapumziko,” amesema Rais Magufuli.

 

Aidha  amewahimiza viongozi na Watanzania kuliweka taifa mikononi mwa Mungu na kumuomba awajalie hekima ili kuwasaidia kupata viongozi wazuri watakaoenda kuwatumikia vema na si viongozi waliokosa maadili wenye lengo la kubomoa taifa.

“Hatuna budi kumuomba Mwenyezi Mungu atupatie viongozi wenye maono, wachapakazi na wazalendo kwa taifa letu tusiangukie mikononi mwa viongozi wabadhirifu,wabinafsi au vibaraka maana kazi ya viongozi kama hao huwa ni kubomoa badala ya kujenga.”

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment