×

Moro: Lori Laangukia Coaster, Watu Kadhaa Wahofiwa Kufa

WATU kadhaa wanahofiwa kufariki dunia kwa kubanwa ndani ya gari baada ya lori kuliangukia basi dogo la abiria (coaster) katika eneo la Nanenane mkoani Morogoro.


 

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu, Agosti 17, 2020, baada trela la lori lenye namba za usajili T 394 BHK kuangukia gari la abiria namba T 149 BNZ linalofanya safari zake kati ya Morogoro na Mbezi jijini Dar es Salaam.

 

 

UPDATES:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema kuwa jumla ya watu 10 wamejeruhiwa kutokana na ajali hiyo ambapo watu wanne ni mahututi wamekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

 

Akizungumza katika ajali hiyo Kamanda wa Jeshi la Polisi Willbroad Mutafungwa amesema tela la Lori hilo lilikatika katika kiunguo cha kichwa na kuangukia coasta hiyo katika maeneo ya Junior Seminary.

 

Kamanda Mutafungwa amewataka Madereva kuwa Makini barabarani huku Juhudi za kumpata dereva wa Lori hilo zinaendelea.

 

Endelea kufuatilia taarifa zetu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Leave a Comment