×

Akaunti ya ‘NBC Shambani’ Yawavutia Wadau wa Korosho  

Mkuuwa Kitengo cha wateja Wadogo na  wa Katikutoka Benki ya NBC  Bw Raymond Urassa akielezeakuhusu huduma mbali mbali za kilimo zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo hudumampya ya ‘NBC Shambani’ mbele ya wadau wa zao korosho nchini wakati wa mkutanomkuu wa wadau hao  uliofanyika  mkoani Lindi hivi karibuni. Benki hiyoilikuwa moja ya wadhamini wakuu wa mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Waziriwa Kilimo Bw Japhet Hasunga.

 

LINDI: Agosti17, 2020: Wadau mbalimbali wa kilimo cha zao la korosho nchini  wameonesha kuvutiwa  na huduma mpya ya NBC Shambani hukuwakibainisha ujio wa huduma hiyo maalumu kwa ajili ya wakulima utaondoachangamoto za muda mrefu  ikiwemokutopata mikopo kwa wakati  sahihi.

 

Wakizungumzawakati walipotembelea banda la huduma za benki hiyo kwenye mkutano mkuu wawadau wa korosho uliofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Lindi, baadhi ya wadau wazao hilo wakiwemo wakulima, wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo nawasafarishaji wa zao hilo walisema miongoni mwa changamoto zinazowakabili kwasasa ni kutopata mikopo kwa wakati sahihi hivyo wanaamini ujio wa huduma hiyompya utaondoa changamoto hiyo.

 

“Lichaya uwepo wa huduma nyingi za kibenki kwa ajili ya wakulima bado tumeendeleakukabiliwa na changamoto kadhaa za huduma za kifedha ikiwemo ucheleweshwaji wamikopo na tunapoipata inakuwa sio wakati sahihi na hivyo kusababisha wengi wetukuitumia kwa matumizi yasiyokusudiwa. Ni matarajio yetu ujio wa huduma NBCShambani utatatua changamoto hii na sisi tupo tayari kuiopokea,’’ alisema BwSalum Muhila, mkulima wa korosho kutoka wilaya ya Liwale, mkoani Lindi.

 

Menejawa Benki ya NBC Tawi la mkoa wa Lindi Bw Iovin Mapunda (Kulia) akizungumza na Bw Salum Muhila, mkulima wa korosho kutoka wilaya ya Liwale, mkoani Lindi kuhusuhuduma za benki hiyo kwa wadau wa kilimo cha korosho ikiwemo huduma mpya yabenki hiyo ya NBC Shambani.

 

Awali,akifafanua kuhusu huduma hiyo kwa wadau hao, Mkuu wa Kitengo cha wateja Wadogona  wa Kati kutoka Benki ya NBC  Bw Raymond Urassa alisema inalenga wadau wotewanaojihusisha na mnyororo wa biashara ya Kilimo wakiwemo wasambazaji wapembejeo za kilimo, wakulima na wasafirishaji wa mazao ya kilimo na tayariimepoanza kutumiwa kwa wingi na wakulima wa zao la ufuta.

 

Alibainishahuduma hiyo inatoa fursa kwa wadau hao kuwa na akaunti ya  vikundi vya wakulima kama vile AMCOS navikundi vingine pamoja na akaunti ya mkulima mmoja mmoja.

 

“Akaunti ya NBC Shambani kwa vikundi vya wakulima inawawezesha kuweka fedha bilaada  ya uendeshaji wa akaunti huku piavikundi vikifaidika kwa  faida nyingiikiwemo kutokatwa gharama za uendeshaji wa akaunti kila mwezi, kupata taarifaza akaunti bure sambamba na kutokatwa makato ya kuhamisha fedha wakati wakulipa wakulima  wenye akaunti NBC,’’alifafanua.

 

Akizungumzakwenye mkutano huo, Waziri wa Kilimo Bw Japhet Hasunga alibainisha kuwa katikakubabiliana na changamoto kadhaa zinazowakabili wakulima ikiwemo kutotambulikarasmi kwenye taasisi za kifedha tayari serikali imeanza kutoa vitambulishomaalum kwa ajili yao vitakavyowatambulisha hususani wanapohitaji huduma zakifedha.

 

“Vitambulishohivyo vya kisasa vitakuwa na ‘chip’ maalumu itakayobeba taarifa zote muhimukuhusu mkulima hatua ambayo tunaamini itazirahisishia taasisi za fedha mlolongomrefu wa kukusanya taarifa za wadau hao na hivyo kuwapatia mikopo kwa wakati,’’alisema Waziri Hasunga ambae katika mkutano huo alikabidhi vitambulisho hivyovya mfano kwa wakulima 15 wa awali.

 

“Zaidipia kwasasa serikali tunatathimini upya sera ya masoko ikiwemo suala zima lakilimo cha mkataba ili wakulima wetu waweze kujua bei za bidhaa zao mapemakabisa,’’ alibainisha.

Leave a Comment