×

Fahamu Eneo Lenye Jina Refu Zaidi Duniani

 

Taumatawhakatangihangakoauauotamateaturipukakapikimaungahoronukupokaiwhenuakitanatahu ni jina la muinuko ulioko Porangahau, New Zealand.

 

Jina hilo likiandikwa kwa urefu linakuwa na alama ‘Characters’ 105: Taumata-whakatangihanga-koauau-o-Tamatea-haumai-tawhiti-ure-haea-turi-pukaka-piki-maunga-horo-nuku-pokai-whenua-ki-tana-tahu.

 

Maana ya jina hilo ni: “eneo ambalo Tamatea, mtu menye magoti makubwa, aliyeteremka, akapanda na kumeza milima, inayojulikana kama ‘mla-ardhi’, akapuliza zumari yake kwa mpendwa wake.”

 

Jina hili limebeba historia ya Legend Taumata ambaye alikuwa akikaa katika mlima huo na kupiga filimbi akiomboleza kifo cha kaka yake aliyeuawa na kabila hasimu la kabila lao.

 

Kwa wale wanaopenda kufanya utalii na wanaopenda kukariri majina ya maeneo wanayotembelea, wanakaribishwa wakariri jina hilo.  Ni ruksa.

 

 

Leave a Comment