×

Waziri Amsimamisha Mkurugenzi Kwa Tuhuma za Ngono

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso.

NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.  leo Agosti 19, 2020,  amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Igunga, Raphael Merumba, na Bodi yake nzima kupisha uchunguzi baada ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kulalamika kuwa anawafanyia unyanyasaji ikiwemo kuwadai rushwa ya ngono.

 

Aweso amefikia maamuzi hayo akiwa ziara mkoani Tabora na kufanya kikao cha ndani na wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Maji Safi mjini Igunga na ndipo walipoanza kumuelezea changamoto wanazokutana nazo ikiwemo Mkurugenzi huyo kuwaomba wafanyakazi wa kike rushwa ya ngono.

 

“Kwahiyo hapa tumepata maelezo ya wafanyakazi lakini kwa kipindi hiki Mkurugrenzi, Mwenyekiti na Bodi yako mtupishe kidogo.  Wakurugenzi wa Mamlaka za Maji msinyanyase wafanyakazi wenu, na kwa yoyote atakayenyanyasa wafanyakazi wake sisi hatutamchekea”, amesema waziri huyo.

Leave a Comment