UONGOZI wa Klabu ya Yanga, Agosti 30, mwaka huu, unatarajia kutambulisha majembe yake mapya katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi.
Kabla ya kufi ka kilele cha tamasha hilo, Jumamosi hii Yanga watalizindua rasmi jijini Dodoma.
Taarifa ambazo Spoti Xtra limezipata kutoka Yanga, zinasema kuwa uongozi umepanga Agosti 30 ndiyo iwe kilele cha Wiki ya Mwananchi ili kutoa fursa kwa mashabiki kuona kikosi chao cha msimu wa 2020/21.
“Tunatara-jia kuwa na mechi ya kimataifa ya kirafiki Agosti 30 katika Uwanja wa Mkapa na ndipo tutakapotambulisha wachezaji wetu wapya wa msimu ujao, kwa sasa timu ipo kambini katika Hotel ya Regency, Mikocheni jijini Dar.
“Tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa wachezaji pamoja na kumleta kocha na ndio maana tulichelewa kutangaza siku hii,” alisema mtoa taarifa.
Miongoni mwa nyota wapya wa Yanga wanaotarajiwa kutambulishwa siku hiyo ni Yacouba Sogne, Yassin Mustapha, Zawadi Mauya, Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto, Waziri Junior, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe.
STORI: KHADIJA MNGWAI, Dar es Salaam


