×

Biden Adai Trump Ameiingiza Nchi Gizani

MGOMBEA urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, Joe Biden, amesema  Rais Donald Trump ameitumbukiza Marekani kwenye giza kwa muda mrefu.

 

Makamu huyo wa rais wa zamani wa Marekani, amesema hali hiyo imesababisha uwepo wa hasira nyingi, hofu na migawanyiko mikubwa miongoni mwa Wamarekani.

 

Biden mwenye umri wa miaka 77, anaingia katika kampeni za uchaguzi huo akiwa anaongoza wazi katika kura za maoni dhidi ya Rais Trump, Lakini zikiwa zimebakia siku 75 kabla ya uchaguzi.

 

Hata hivyo, Rais Donald Trump wa chama cha Republican ana muda wa kutosha kubadili matokeo ya kura za maoni.

Leave a Comment