VIDEO vixen matata Bongo, Nelly Kamwelu amefunguka kuwa, anatamani mno kuzaa ila amejifunza kuwa mtoto bila malezi ya baba ni tatizo.
Akistorisha na IJUMAA SHOWBIZ, Nelly amesema kuwa, anapenda mno watoto na kuna kipindi anatamani kubeba mtoto wake mwenyewe, lakini hawezi kufanya hivyo bila kuingia kwenye ndoa
.“Kiukweli natamani sana kuzaa, lakini nimejiwekea malengo kuwa siwezi kufanya hivyo bila kuwa kwenye ndoa, raha ya malezi muwe wawili,” anasema Nelly ambaye pia ni mwanamitindo wa kimataifa.

