×

Maelfu Waandamana Kumtaka Lukashenko Aachie Madaraka

KIONGOZI wa upinzani nchini Belarus, Svetlana Tikhanovskaya, amewataka waandamanaji wanaodai demokrasia kuendelea na juhudi hizo, akisema Rais Alexander Lukashenko hana “chaguo” ila kuzungumza na upinzani.

 

Katika mahojiano na shirika la habari la AFP, Tikhanovskaya pia amesema watu wa Belarus wameondoa hofu yao na kuiita hatua ya Lukashenko ya kuongeza usalama katika mipaka kuwa ni juhudi tu za kutaka “kuondoa mtazamo katika matatizo ya ndani ya nchi hiyo”.

 

Wapinzani wa  Lukashenko  wanaendelea kuandamana katika taifa hilo la zamani la Umoja wa Kisovieti kupinga kuchaguliwa kwake tena na wanadai ajiuzulu.

Leave a Comment