×

Samia Azungumza na Wajumbe Tume ya Haki za Binadamu

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kazi nzuri inayofanywa kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi na kuweza kupata haki zao pale wanapodhulumiwa.

 

Amesema hayo alipokutana na ujumbe wa makamishna wa tume hiyo na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, walipomtembelea kwenye makazi yake Kilimani jijini Dodoma.

Samia meipongeza tume hiyo kwa  kubadilika na kufanya kazi vizuri pamoja na kutenda haki kwa wananchi na taasisi zote kwa ujumla.

 

Naye Mwenyekiti wa tume hiyo, Mathew Mwaimu,  ameipongeza serikali kwa  kuwaletea wananchi maendeleo bora na kuitakia kila la heri katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

 

Amesema tume yake haipendezewi na vitendo vya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ambao wamekuwa wakisema watu badala ya kunadi sera za vyama vyao.

Leave a Comment