×

Hotuba ya Ruto Yazua Gumzo: Atoa Ujumbe Mzito kwa Watanzania na Wakenya – Video

Rais wa Kenya, William Ruto, amesema kuwa wananchi wa Kenya na Tanzania si maadui, bali wanakabiliwa na changamoto zinazofanana ambazo zinahitaji ushirikiano wa pamoja kuzitatua.

Akihutubia Bunge la Tanzania leo Jumanne, Mei 5, 2026, Rais Ruto alisisitiza kuwa adui mkubwa wa mataifa hayo mawili si tofauti zao za kitaifa, bali ni umaskini, ukosefu wa ajira na kipato kwa wananchi wake.

“Wakenya siyo maadui wa Tanzania na Watanzania siyo maadui wa Kenya. Adui wetu sote ni pale ambapo hatuna mali, hatuna nafasi za ajira na hatuna fedha hiki ndicho kinachotutesa,” alisema.

Katika hotuba yake, Ruto alieleza kuwa Afrika Mashariki ina fursa kubwa ya kiuchumi endapo nchi zake zitaimarisha mshikamano na kushirikiana kwa karibu zaidi. Alionya dhidi ya kujenga taswira ya ushindani usio na manufaa kati ya mataifa jirani, akisema hali hiyo inaweza kudhoofisha juhudi za maendeleo.

Badala yake, aliwataka viongozi na wananchi kuzingatia kuunda mazingira bora ya uwekezaji, kuongeza ajira kwa vijana, na kuboresha kipato cha wananchi kupitia sera shirikishi za kikanda.

Rais Ruto alihitimisha kwa kusisitiza kuwa mustakabali wa wananchi wa Afrika Mashariki uko kwenye umoja, akieleza kuwa kwa kushirikiana, mataifa hayo yanaweza kushinda changamoto za kiuchumi na kujenga ustawi wa pamoja kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Leave a Comment